Katika nyenzo zake za kujaribu kutoa majibu ya swali la kale, “Maisha ni nini?” mwandishi anatafiti maumbile na jinsi nguvu za maisha zilizomo katika ulimwengu kwa kutokana na misimamo ya dini ya Budha akilinganisha mara kwa mara na ukweli wa sayansi pamoja na uzindushi wa kifalsafa kutoka katika tamaduni za Magharibi ma Mashariki.
Anadadisi dhana zinazohusu mwili na roho, mwandadamu na maumbile, nafsi isiyobadilika, fumbo la wakati pamoja na maana na upeo wa ulimwengu safidi, yaani ulimwengu mzima wenye taratibu maalum. |